Jumamosi, 29 Machi 2014

HIVI NDIVYO RAIS KIKWETE NA CHAMA CHAKE WANAVYOTEKETEZA MABILIONI YA WALIPA KODI KUTOKANA NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA SOMA KWA MAKINI MAKALA HII

Na Karoli Vinsent
http://umwezi.net/wp-content/uploads/2013/06/Jakaya-Kikwete.jpg
HOFU ya Mabilioni ya walipa kodi kupotea bure kutokana na Mchakato wa katiba mpya yabainika,hii inatoka Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Wiki iliyopita bungeni huku akionekana kufanya usaliti mkubwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba huku akiyafuata matakwa ya chama chake cha CCM.

Hofu hii ya mabilioni ya Wananchi walalahoi kupotea inatoka na kupata katiba mpya yenye kuwanufaisha viongozi kama Rais Kikwete na Chama chake cha CCM na sio wananchi walalahoi wa Tanzania.

Rais Kikwete juzi wakati anahutubia Wajumbe bungeni alionekana wazi kiongozi huyo kuwasaliti watanzania,huku akishindwa kuwaachia wajumbe ambao zaidi ya 600 kuamua hatma ya katiba badala yake yeye ndio kuamua mchakato mzima wa katiba.

Wachambuzi mbalimbali waliozungumza na mwandishi wa Mtandao huu wengi walihoji hata uwezo wa kiongozi huyo mkubwa wa nchi kitaaluma, baada ya kuonekana wazi kuboronga katika mchakato mzima wa katiba.

Mchambuzi ambaye ametoka Chuo Kikuu cha Dodoma Seiph Yahaya ambaye kwa upande wake alimshangaa Rais Kikwete kuonekana kufanya usaliti mkubwa kwenye tume iliyotumia pesa nyingi za walipaka kodi na kuonekana sawa na bure.

Yahaya ambaye ni Msomi wa Shahada ya juu masuala ya Sayansi ya siasa alisema ni Dhahiri Shairi Rais Kikwete hana nia njema kwa watanzania kupata katiba mpya badala yake alikurubuka tu kuanzisha mchakato huu,

huku akisahau kwamba watanzania walimwamini kama kiongozi atakayekumbukwa kwenye historia lakini kwa ishara  hii amejichafua kwa wananchi alisema mchambuzi huyo.

Usaliti wa Rais Kikwete kwenye mchakato huu Wa katiba mpya ulionekana wazi wakati alipokuwa anateua wajumbe 201,ambapo katika  uteuzi huu aliwajaza makada wenzake wa Chama cha Mapinduzi,huku akiwaacha watu muhimu kutoka kwa wananchi.

Wamejazana bungeni kana kwamba wanatunga katiba ya chama chao, wanataka kuumeza mchakato huu. Sina shaka tuendako si kwema.
     Najua wanasiasa wengi hivi sasa wanawaza madaraka tu ndiyo maana hata Rais Kikwete hataki wananchi wawe na nguvu ya kuwaondoa wabunge wao wanaovurunda.
Wanataka katiba itungwe kulinda masilahi yao na wala si ya nchi. Huu ni udhaifu mkubwa sana!
      Je Rais Kiwete ulivyokuwa unawaambia Makada wa Chama chako wajiandae kisakrojia kutokana na mchakato huu wa katiba kumbe hata wewe ulikuwa ujajiandaa kisakrojia ndio maana umeamua kuvuruga mchakto mzima wa katiba.
    Je hivi unataka tuanze kumwamini Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, alishatuambia mapema kuwa hakuna haja ya kuandika Katiba mpya bali tuiwekee viraka hii tuliyonayo, huyu leo hii ni miongoni mwa wanaosimamia uandikwaji wa Katiba mpya, je, lini ameona kuna umuhimu wa kuwa na mpya?
Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani, alipinga mchakato kuandika Katiba mpya lakini hivi sasa naye yumo bungeni, anashiriki katika kile asichokiamini.
      Naandika makala hii kwa uchungu huku nikihoji Makada wa CCM, chama ni muhimu zaidi kuliko masilahi ya taifa, wako tayari kuuhujumu mchakato wa katiba mpya ilmradi mazingira ya kufanya ujanja ujanja nyakati za uchaguzi yaendelee kuwepo.
Makada wa aina hii wako tayari kufumbia macho uvunjwaji wa Katiba ya Muungano uliofanywa na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 ilimradi chama chao kiwe salama.
        Je hata kwa Tafsiri hii tunahaja ya kumkumbuka Rais wetu akiondoka madarakani kwa wema?wakati mabilioni ya walipa kodi yanapotea kutokana na mchakato huu wa katiba mpya?
Nawasubiri hawa wajumbe wa Bunge maalumu la Katiba, wachanganye akili za kuambiwa na zao, nasubiri kuvunjika kwa Bunge hili wakati wowote kuanzia sasa.
          Najua ni lazima litavunjika tu, ni suala la muda tu, litavunjika kwa sababu lilianza bila maridhiano, lilianza kwa mguu mbaya, ambapo wajumbe wengi wamebeba misimamo ya vyama na makundi yao badala ya masilahi ya taifa.
Tafakari.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni