Na Karoli Vinsent
HOFU ya Mabilioni ya walipa
kodi kupotea bure kutokana na Mchakato wa katiba mpya yabainika,hii inatoka Hotuba
ya Rais Jakaya Kikwete Wiki iliyopita bungeni huku akionekana kufanya usaliti mkubwa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba huku akiyafuata matakwa ya chama chake cha CCM.
Hofu hii ya mabilioni ya
Wananchi walalahoi kupotea inatoka na kupata katiba mpya yenye kuwanufaisha
viongozi kama Rais Kikwete na Chama chake cha CCM na sio wananchi walalahoi wa Tanzania.
Rais Kikwete juzi wakati
anahutubia Wajumbe bungeni alionekana wazi kiongozi huyo kuwasaliti
watanzania,huku akishindwa kuwaachia wajumbe ambao zaidi ya 600 kuamua hatma ya
katiba badala yake yeye ndio kuamua mchakato mzima wa katiba.
Wachambuzi mbalimbali
waliozungumza na mwandishi wa Mtandao huu wengi walihoji hata uwezo wa kiongozi
huyo mkubwa wa nchi kitaaluma, baada ya kuonekana wazi kuboronga katika
mchakato mzima wa katiba.
Mchambuzi ambaye ametoka Chuo
Kikuu cha Dodoma Seiph Yahaya ambaye kwa upande wake alimshangaa Rais Kikwete
kuonekana kufanya usaliti mkubwa kwenye tume iliyotumia pesa nyingi za walipaka
kodi na kuonekana sawa na bure.
Yahaya ambaye ni Msomi wa
Shahada ya juu masuala ya Sayansi ya siasa alisema ni Dhahiri Shairi Rais
Kikwete hana nia njema kwa watanzania kupata katiba mpya badala yake alikurubuka
tu kuanzisha mchakato huu,
huku akisahau kwamba
watanzania walimwamini kama kiongozi
atakayekumbukwa kwenye historia lakini kwa ishara hii amejichafua kwa wananchi alisema mchambuzi
huyo.